Zuma aondoa kesi ya kupinga ripoti mahakamani

0
26

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesitisha jitihada zake kwa njia ya mahakama, kuzuia kutolewa kwa ripota iliyotengenezwa na aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kupambana na rushwa Thuli Madonsela.

jacob-zuma-resign

Madonsela alifanya uchunguzi kuhusu madai kuwa Zuma aliruhusu familia tajiri ya Gupta kuwa na ushawishi mkubwa serikalini.

Wakili wa Bw.  Zuma aliiambia mahakama ya juu mjini Pretoria kuhusu uamuzi huo lakini sababu yake bado haijulikani.

Makundi ya upinzani yanafanya maandamano kwenye miji mkubwa nchini Afrika kusini kupinga uongozi wa rais Jacob Zuma.

Maelfu ya watu wako mji mkuu Pretoria wakimtaka Zuma ajiuzulu. Ripoti hiyo inaaminiwa kuwa na lawama za kumharibia jina Bw.  Zuma.

Hatua ya Zuma ya kuzuia kutolewa kwa ripoti hiyo zilipingwa na vyama vya upinzani ambavyo sasa vinataka alipie gharama ya kesi.

Bado haibainiki ni lini ripoti hiyo ilitolewa rasmi kwa umma. Bw. zuma amekumbwa na madai yanayohusu ufisadi kwa zaidi ya miaka kumi.

 

 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY