Umoja wa Mataifa kupiga mbiu huku raia kukimbia mashambulizi Aleppo .

0
15

 

Raia zaidi ya 16,000 wameondolewa katika makazi yao na serikali ya Syria katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa mji wa Aleppo, Umoja wa Mataifa anasema.

Shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria limesema kwamba kiasi ya raia 27,000 wamekimbia makaazi yao baada ya majeshi ya Syria kukamata karibu theluthi ya eneo la mashariki mwa Aleppo linalodhibitiwa na waasi.

Na kwa mujibu wa wabunge walioko karibu na serikali ya Syria , wapiganaji waasi 484 wamesalim amri mashariki mwa Aleppo. Wapiganaji hao ambao si wapiganaji wa kundi la Nusra Front ama Ahrar al Sham ama makundi ya jihadi, walikabidhi silaha zao pamoja na wao wenyewe kwa jeshi la Syria.

Maelfu ya wakaazi waliingia katika maeneo yanayoshikiliwa na Wakurdi na serikali jana wakati maeneo ya waasi katika eneo la kaskazini la wilaya iliyozingirwa ya mashariki mwa Aleppo ikiangukia mikononi mwa majeshi ya serikali.

SHARE

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY