Mwisho wa boko haram – Rais Buhari

0
24
Muhammadu Buhari, former Nigerian military ruler and presidential candidate for the Congress for Progressive Change (CPC) speaks during an interview with Reuters at a private residence in Lagos February 19, 2011. Buhari, the main opposition candidate in Nigeria's presidential election, said he was optimistic it would be a more credible race than in the past but warned events in north Africa showed people would no longer accept a rigged vote. Picture taken February 19, 2011. To match Interview NIGERIA-BUHARI/ REUTERS/Akintunde Akinleye (NIGERIA - Tags: POLITICS HEADSHOT)

Rais Muhammadu Buhari, ambaye kwa sasa yupo mjini Dakar, Senegal, amewahakikishia jumuiya ya kimataifa kwamba mwisho wa kikundi cha kigaidi, boko haram, hiko ukingoni.

Akizungumza katika Jopo la Wakuu wa Nchi katika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa mjini Dakar  juu ya Amani na Usalama barani Afrika, Rais pia aliwapa uhakika jumuiya ya kimataifa kwamba hali ya usalama nchini Nigeria imepanda kwa kiasi kikubwa.

“Mwezi mmoja uliopita, nilizungumza na Rais wa Chad na mimi nilivutiwa kwamba idadi ya Wachadi na Wanigeria waliokuwa wanachama wa boko haram wanajisalimisha kwake kwa uwingi. Habari njema ni kwamba mwisho wa msimu wakukimbizana ushafika ukingoni katika kanda ya Kaskazini mashariki mwa Nigeria. “

Kiongozi huyo wa Nigeria pia aliiwapongeza nchi jirani kwa kuunga mikono katika mapambano dhidi ya uasi.

“Wanachama wa Muungano wa Kikosi kazi ya Taifa (MNJTF) wako katika kazi  zao na katika makubaliano wao watasonga kuona mwisho wa Boko haram . Kwa sasa tunaoporeti katika msitu wa Sambisa na tunavyo tambuwa katika eneo la Bonde la Ziwa Chad hakuna Boko haram, nadhani wame kamilisha kazi , “Rais alisema.

Akionyesha baadhi ya mafanikio ya ushirikiano miongoni mwa Tume ya nchi zilioko katika Bonde la  Ziwa Chad akiwemo Chad, Niger, Cameroon,Jamuhuri ya  Benin na Nigeria, kiongozi wa Nigeria aliiambia mkutano kwamba boko haram haishikilii tena wilaya yoyote au eneo za  Serikali za Mitaa (LGA) katika nchi yake .

“Wale ambao wanaishi katika Majimbo ya Kaskazini mashariki wanajua kwamba boko haram hawana imaa yeyote katika  Halmashauri 774 nchini Nigeria. Lakini wana  mfumo wa kutumia  wasichana wengi wenye umri mdogo na kuwatuma kama chambo kwa makanisa, misikiti na maeneo ya soko. Hiyo pia kwa sasa imekuwa nadra sana. Nadhani boko haram wamejipiga wenyewe risasi za mguu kwa kutumia itikadi zao potofu kusingizia dini wakati wana waua watoto katika shule zao, watu katika msikiti na makanisa na kupiga kelele Allahu Akbar, “Rais aliongeza.

SHARE

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY