Miripuko miwili yauwa kiasi watu 10 Mogadishu

0
9

Watu wanane wameuawa katika mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga yaliyoilenga kwa wakati unaokaribiana hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Kwanza gari limeripuka kwenye kizuizi cha barabarani karibu ya uwanja wa ndege na kuwauwa maafisa kadhaa wa usalama, na baadaye kidogo lori likapita kwa kasi katika kizuizi hicho, na kuripuka karibu ya Peace Hotel, ambayo inapendelewa na watalii pamoja na maafisa wa serikali.

Mripuko huo umeiharibu sehemu moja ya jengo la hoteli hiyo. Kundi la itikadi kali za kiislamu, al-Shabab ambalo linapigana kuiondoa madarakani serikali inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, limedai kuhusika na shambulio hilo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY