Viongozi wa ECOWAS kuongoza mazungumzo kuhusu Gambia

0
12
Viongozi wa ECOWAS , Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Rais zamani wa Ghana John Mahama

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anandaa mkutanao wa viongozi wanne wa nchi za Afrika Magharibi baadaye katika jitihada za kuzuia kutokea ghasia nchini Gambia.

Viongozi wa ECOWAS , Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Rais zamani wa Ghana John Mahama
Viongozi wa ECOWAS , Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Rais zamani wa Ghana John Mahama

Hii ni baada ya Rais Yahya Jammeh amekataa koundoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.

Rais wa Senegal Macky Sall, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Makamu Rais wa Sierra Leone Victor Foh pamoja na aliyekuwa Rais wa Ghana John Mahama walisafiri kwenda Abuja kwa Mazungumzo.

Bwana Buhari na Rais wa zamani wa ghana John Mahama pia wamepewa jukumu na Jumuia ya nchi za Afrika Magharibi, Ecowas, kuhakikisha usalama wa mshindi wa uchaguzi Adama Barrow, na pia kuhakikisha kuwepo upokezanaji wa amani wa mamlaka. tarehe 9 mwezi Januari.

Bwana Buhari na viongozi wengine wa nchi za Afrika Magharibi walimtembelea Bwana Jammeh mwezi uliopita lakini hawakufanikiwa kumshawishi kuondoka madarakani

Maafisa wa Ecowas wanasema kuwa hatua za kijeshi za kumlazimisha Jammeh kuondoka madarakani zinafanyiwa tathmini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY